IDARA YA KISWAHILI

Kiswahili ni idara ndogo chini ya idara kuu ya lugha (Languages). Idara hii inashughulikia somo la Kiswahili pekee katika shule. Somo hili lina umuhimu mkubwa kwani ni mojawapo ya masomo matano yanayozingatiwa kama kigezo cha kufuzu kwa kozi yoyote baada ya masomo ya shule ya Upili.
Idara hii imeweka mikakati na mbinu kabambe za kuwatayarisha wanafunzi kuimarika katika somo hili. Matayarisho haya sio tu ya kufuzu masomoni bali pia kuwapa wanafunzi msingi dhabiti kwa taaluma/ajira wanazopania kuziendeleza kama vile ualimu, uhariri, uandishi wa vitabu, utangazaji, uhariri wa Makala mbali mbali, na kadhalika.
Mikakati na mbinu  zinazotumiwa shuleni kuandaa wanafunzi ni pamoja na mijadala, utangazaji wa habari, uandishi na ukariri wa mashairi katika hafla mbalimbali, ulumbi, uandishi wa jarida la shule, uimbaji wa nyimbo, usanii, ma kadhalika. 
Somo la Kiswahili limesheni vipera tofauti tofauti vinavyokuza na kuimarisha wanafunzi katika stadi mbalimbali, Kwa mfano, kipera cha Fasihi Andishi huwatayarisha wanafunzi kuhakiki na kuchochea ari ya uandishi wa vitabu na Makala magazetini kwa lugha hii muhimu. Kwa upande mwingine, kipera cha Isimu Jamii huwafaa wanafunzi katika uelewa wao wa matumizi ya lugha katika miktadha tofauti ya jamii. Kipera cha Insha  huchochea stadi ya Uandishi na ubunifu katika maswala mbalimbali. 
Kwa muhtasari, somo la Kiswahili ni aali katika mfumo mzima wa kumchonga mwanafunzi ili ainuke kuwa raia mkamilifu wa Nchi ya Kenya. Njoo tuendeleze lugha ashirafi (tukufu) ya Kiswahili.
Bi. Caroline Wanyonyi
Mkuu wa Idara ya Kiswahili.

Kiswahili ni idara ndogo chini ya idara kuu ya lugha (Languages). Idara hii inashughulikia somo la Kiswahili pekee katika shule. Somo hili lina umuhimu mkubwa kwani ni mojawapo ya masomo matano yanayozingatiwa kama kigezo cha kufuzu kwa kozi yoyote baada ya masomo ya shule ya Upili.

Idara hii imeweka mikakati na mbinu kabambe za kuwatayarisha wanafunzi kuimarika katika somo hili. Matayarisho haya sio tu ya kufuzu masomoni bali pia kuwapa wanafunzi msingi dhabiti kwa taaluma/ajira wanazopania kuziendeleza kama vile ualimu, uhariri, uandishi wa vitabu, utangazaji, uhariri wa Makala mbali mbali, na kadhalika.

Mikakati na mbinu  zinazotumiwa shuleni kuandaa wanafunzi ni pamoja na mijadala, utangazaji wa habari, uandishi na ukariri wa mashairi katika hafla mbalimbali, ulumbi, uandishi wa jarida la shule, uimbaji wa nyimbo, usanii, ma kadhalika. 

Somo la Kiswahili limesheni vipera tofauti tofauti vinavyokuza na kuimarisha wanafunzi katika stadi mbalimbali, Kwa mfano, kipera cha Fasihi Andishi huwatayarisha wanafunzi kuhakiki na kuchochea ari ya uandishi wa vitabu na Makala magazetini kwa lugha hii muhimu. Kwa upande mwingine, kipera cha Isimu Jamii huwafaa wanafunzi katika uelewa wao wa matumizi ya lugha katika miktadha tofauti ya jamii. Kipera cha Insha  huchochea stadi ya Uandishi na ubunifu katika maswala mbalimbali. walimu waliopo kwenye Idara hii ni kama wafuatao: 

1. BI. CAROLINE SIMIYU  - MKUU WA IDARA

2. BI. PATSY MAITANO     - MWANACHAMA

3. BW. RICHARD GACHOKA - MWANACHAMA

4. BW. SAMSON KEYAH       - MWANACHAMA

Kwa muhtasari, somo la Kiswahili ni aali katika mfumo mzima wa kumchonga mwanafunzi ili ainuke kuwa raia mkamilifu wa Nchi ya Kenya. Njoo tuendeleze lugha ashirafi (tukufu) ya Kiswahili.Bi. Caroline WanyonyiMkuu wa Idara ya Kiswahili.

ENVIRONMENTAL CLUB

The environmental club is one of the vibrant clubs in the school. The aim of the club is to ensure that the society lives and carry out their …

read more

SCIENCE DEPARTMENT

Vision To produce a scientific community that is beneficial to society and encourage the development and promotion of scientific ideas and …

read more